Header Ads

BARCELONA BILA MESSI KUWAVAA BAYER LEO LIGI YA MABINGWA ULAYA.



Jumanne Septemba 29, 2015

Barcelona Vs Bayer 04 Leverkusen

BATE Borisov Vs Roma

FC PortoVs Chelsea

Bayern Munich Vs Dinamo Zagreb

Arsenal Vs Olympiakos

Lyon Vs Valencia CF

Maccabi Tel Aviv Vs Dynamo Kyiv

Zenit St Petersburg Vs AA Gent

Jumatano Septemba 30, 2015

FC Astana v Galatasaray

CSKA Moscow Vs PSV

Juventus Vs Sevilla

Borussia Monchengladbach Vs Manchester City

Malmo FF Vs Real Madrid

Manchester United Vs VfL Wolfsburg

Atletico MadridVs Benfica

Shakhtar Donetsk Vs Paris Saint-Germain

HATUA ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, inaendelea leo na kesho, huku mabingwa watetezi, Barcelona wakiikaribisha Bayer 04 Leverkusen Uwanja wa Camp Nou mjini Barcelona, Hispania.

Katika mchezo huo, Barcelona watamkosa nyota wake, Lionel Messi aliyeumia mwishoni mwa wiki katika mchezo wa La Liga ikishinda 2-1 dhidi ya Las Palmas Barcelona, lakini hapana shaka Neymar na Luis Suarez watawabeba wababe hao wa Katalunya.

BATE Borisov watakuwa wenyeji wa Roma Uwanja wa Borisov Arena, Chelsea wataifuata FC Porto Uwanja wa DragaoBayern Munchen wataikaribisha Dinamo Zagreb Uwanja wa Allianz Arena, Arsenal wataikaribisha Olympiakos Uwanja wa Emirates, Lyon wataikaribisha Valencia Uwanja wa Stade de Gerland, Maccabi Tel Aviv wataikaribisha Dynamo Kyiv Uwanja wa Bloomfield na Zenit St Petersburg wataikaribisha KAA Gent  Uwanja wa Petrovski.

Messi aliumia mwishoni mwa wiki katika mchezo wa La Liga ikishinda 2-1 dhidi ya Las Palmas Barcelona


Michuano hiyo itaendelea kesho FC Astana ikiikaribisha Galatasaray Uwanja wa Astana Arena, CSKA Moscow ikiikaribisha PSV Uwanja wa Arena Khimki, Juventus ikiikaribisha Sevilla Uwanja wa Juve, Borussia Monchengladbach ikiwakaribisha Manchester City Uwanja wa Borussia-Park, Malmo FF ikiwakaribisha Real Madrid Uwanja wa Swedbank, Manchester United ikiwakaribisha VfL Wolfsburg Uwanja wa Old Trafford Atletico de Madrid ikiwakaribisha Benfica Uwanja wa Vicente Calderon na Shakhtar Donetsk wakiwakaribisha Paris Saint-Germain Uwanja wa Lviv. 

No comments

Powered by Blogger.