STARS YA KUIVAA MALAWI YA TAJWA.
KIKOSI cha timu ya soka ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars kitakachoikabili Malawi, The Flames katika mechi ya kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia 2018, kimetangazwa kikiwa hakina mabadiliko na kilichoikabili Nigeria katika kuwania kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika 2017.
Aidha, katika kikosi hicho, mshambuliaji nyota wa zamani wa Yanga, Mrisho Ngassa atachelewa kujiunga na timu hiyo baada ya kuombewa udhuru na kikosi chake cha Free State Stars ya Afrika Kusini.

Kwa mujibu wa Kocha Msaidizi wa Taifa Stars, Hemed Morocco ametaja kikosi kwa ajili ya mchezo dhidi ya Malawi mwezi ujao, lakini Ngassa ameombewa udhuru. Free State Stars ya Ligi Kuu ya Afrika Kusini imemuombea udhuru Ngassa achelewe kidogo kujiunga na kambi ya maandalizi ya mchezo huo.
Free State imewaandikia Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuomba Ngassa ajiunge na kambi baada ya Oktoba 4, akimaliza kuichezea katika mchezo wa Kombe la Telkom Knockout dhidi ya Bidvest Wits siku moja kabla.
Morocco aliyetaja kikosi hicho badala ya Kocha Mkuu, Charles Boniface Mkwasa ambaye amekwenda Iringa kwenye msiba wa mama mkwe, amesema kikosi kitaingia kambini Oktoba mosi.
Taifa Stars inatarajiwa kumenyana na The Flames Oktoba 10, mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam katika mchezo wa kwanza kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi.
Katika kikosi hicho cha Stars amemwita kipa wa Mtibwa Sugar, Said Mohamed ambaye hakuwamo katika kikosi kilichoikabili Nigeria mapema mwezi huu. Makipa wengine ni Aishi Manula (Azam FC) na Ally Mustafa (Yanga).
Mabeki walioitwa ni Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ (Simba), Juma Abdul (Yanga), Shomary Kapombe (Azam FC), Mwinyi Mngwali (Yanga), Hassan Isihaka (Simba), Kelvin Yondani (Yanga) na nahodha Nadir Haroub (Yanga).
Viungo ni Himid Mao (Azam FC), Said Ndemla (Simba), Salum Telela (Yanga), Frank Domayo (Azam FC), Mudathir Yahya (Azam FC), Simon Msuva (Yanga) na Deus Kaseke (Yanga). Washambuliaji ni Rashid Mandawa (Mwadui FC), John Bocco (Azam FC), Ngassa (Free State Stars, Afrika Kusini), Mbwana Samatta (TP Mazembe, DRC), Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC) na Farid Mussa (Azam FC).
No comments