Header Ads

OTAMEND KUCHAFUA HALI YA HEWA

Sentahafu wa Valencia Nicolas Otamendi anayewaniwa na Manchester United, amezidi kuwa gumzo baada ya kuenguliwa kwenye uzinduzi wa sare mpya za timu hiyo. 

Mkali huyo wa kimataifa wa Argentina mwenye umri wa miaka 27, amekuwa akihusishwa na usajili wa kwenda Old Trafford kwa kipindi chote cha dirisha hili la usajili. Valencia wakatupia kwenye ukurasa wao wa Twitter picha ya wachezaji wake wakiwa wametinga jezi mpya huku Otamendi pamoja na umuhimu wake wote lakini hakuonekana pichani. Pamoja na kwamba ni mapema mno kutafsiri kutokuwepo kwa Otamendi  kwenye uzinduzi huo, lakini hiyo inazidi kukoleza moto wa safari yake ya Manchester United. 

No comments

Powered by Blogger.